15 Kisha Mwenyezi-Mungu alimwambia Yoshua,
16 “Waamuru makuhani wanaobeba sanduku la maamuzi, watoke mtoni Yordani.”
17 Basi, Yoshua akawaamuru wale makuhani, “Tokeni mtoni Yordani.”
18 Hao makuhani waliokuwa wamebeba lile sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu walipotoka katikati ya mto Yordani, na kukanyaga ukingo wa mto, maji ya mto Yordani yakaanza kutiririka tena, na kufurika kama kwanza.
19 Waisraeli walivuka mto Yordani katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi huko mjini Gilgali, mashariki ya Yeriko.
20 Yoshua akayasimika yale mawe kumi na mawili ambayo waliyachukua kutoka mtoni Yordani, huko Gilgali.
21 Kisha Yoshua akawaambia Waisraeli, “Watoto wenu watakapowaulizeni siku zijazo, ‘Je, mawe haya yana maana gani?’