6 Naye akaniambia pia niseme neno hili la Mwenyezi-Mungu kumhusu Zerubabeli: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Huwezi kushinda kwa nguvu au kwa uwezo wako mwenyewe, bali kwa msaada wa roho yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”
7 Tena, akaongeza kusema: “Je, mlima huu ni kizuizi? La! Wewe Zerubabeli utausawazisha. Wewe utaanzisha ujenzi mpya wa hekalu, na wakati utakapoliweka jiwe la mwisho, watu watashangilia wakisema, ‘Ni zuri! Naam, ni zuri!’”
8 Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia:
9 “Zerubabeli ameuweka msingi wa hekalu naye pia atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao.
10 Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”