Zekaria 9 BHN

Hukumu juu ya mataifa jirani

1 Kauli ya Mwenyezi-Mungu:Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadrakibali pia dhidi ya Damasko.Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu,kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli.

2 Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki;na hata miji ya Tiro na Sidoniingawaje yajiona kuwa na hekima sana.

3 Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa,umejirundikia fedha kama vumbi,na dhahabu kama takataka barabarani.

4 Lakini Bwana ataichukua mali yake yote,utajiri wake atautumbukiza baharini,na kuuteketeza mji huo kwa moto.

5 Mji wa Ashkeloni utaona hayo na kuogopa,nao mji wa Gaza utagaagaa kwa uchungu;hata Ekroni, maana tumaini lake litatoweka.Mji wa Gaza utapoteza mfalme wake,nao Ashkeloni hautakaliwa na watu.

6 Mji wa Ashdodi utakaliwa na machotara.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kiburi cha Filistia nitakikomesha.

7 Nitawakomesha kula nyama yenye damu,na chakula ambacho ni chukizo.Mabaki watakuwa mali yangu,kama ukoo mmoja katika Yuda.Watu wa Ekroni watakuwa kama Wayebusi.

8 Mimi mwenyewe nitailinda nchi yangu,nitazuia majeshi yasipitepite humo.Hakuna mtu atakayewadhulumu tena watu wangu,maana, kwa macho yangu mwenyewe,nimeona jinsi walivyoteseka.”

Mfalme wa amani

9 Shangilieni sana enyi watu wa Siyoni!Paazeni sauti, enyi watu wa Yerusalemu!Tazama, mfalme wenu anawajieni,anakuja kwa shangwe na ushindi!Ni mpole, amepanda punda,mwanapunda, mtoto wa punda.

10 Atatokomeza magari ya vita nchini Efraimu,na farasi wa vita kutoka mjini Yerusalemu;pinde za vita zitavunjiliwa mbali.Naye ataleta amani miongoni mwa mataifa;utawala wake utaenea toka bahari hata bahari,toka mto Eufrate hata miisho ya dunia.

Kurudishwa kwa watu wa Mungu

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa sababu ya agano langu nanyi,agano lililothibitishwa kwa damu,nitawakomboa wafungwa wenuwalio kama wamefungwa katika shimo tupu.

12 Enyi wafungwa wenye tumaini;rudini kwenye ngome yenu.Sasa mimi ninawatangazieni:Nitawarudishieni mema maradufu.

13 Yuda nitamtumia kama uta wangu;Efraimu nimemfanya mshale wangu.Ee Siyoni! Watu wako nitawatumia kama upangakuwashambulia watu wa Ugiriki;watakuwa kama upanga wa shujaa.”

14 Mwenyezi-Mungu atawatokea watu wake;atafyatua mishale yake kama umeme.Bwana Mwenyezi-Mungu atapiga tarumbeta;atafika pamoja na kimbunga cha kusini.

15 Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawalinda watu wake,nao watawaangamiza maadui zao.Watapiga kelele vitani kama waleviwataimwaga damu ya maadui zao.Itatiririka kama damu ya tambikoiliyomiminwa madhabahuni kutoka bakulini.

16 Wakati huo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, atawaokoa,maana wao ni kundi lake;nao watang'aa katika nchi yakekama mawe ya thamani katika taji.

17 Jinsi gani uzuri na urembo wake ulivyo!Wavulana na wasichana watanawirikwa wingi wa nafaka na divai mpya.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14