Zekaria 10 BHN

Mungu anaahidi ukombozi

1 Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika.Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua;ndiye awapaye watu mvua za rasharasha,na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.

2 Vinyago vyao vya kupigia ramli ni upuuzi mtupu,na waaguzi wao wanaagua uongo;watabiri wao wanatabiri ndoto za danganyifu,na kuwapa watu faraja tupu.Ndio maana watu wa Yuda wanatangatanga kama kondoo;wanataabika kwa kuwa wamekosa mchungaji.

3 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nimewaka hasira dhidi ya hao wachungaji,nami nitawaadhibu hao viongozi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi,nitalitunza kundi langu, ukoo wa Yuda.Nitawafanya kuwa farasi wangu hodari wa vita.

4 Kwa ukoo wa Yuda kutatokea:Watawala wa kila namna,viongozi imara kama jiwe kuu la msingi,walio thabiti kama kigingi cha hema,wenye nguvu kama upinde wa vita.

5 Watu wa Yuda watakuwa kama mashujaa vitaniwatawakanyaga maadui zao katika tope njiani.Watapigana kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu nipo pamoja nao;nao watawaaibisha hata wapandafarasi.

6 “Watu wa Yuda nitawaimarisha;nitawaokoa wazawa wa Yosefu.Nitawarejesha makwao kwa maana nawaonea huruma,nao watakuwa kana kwamba sikuwa nimewakataa.Mimi ni Mwenyezi-Mungu, Mungu wao,nami nitayasikiliza maombi yao.

7 Watu wa Efraimu watakuwa kama mashujaa vitani;watajaa furaha kama waliokunywa divai.Watoto wao wataona hayo na kufurahi,watajaa furaha mioyoni kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu.

8 “Nitawaita watu wanguna kuwakusanya pamoja;nimekusudia kuwakomboa,nao watakuwa wengi kama hapo awali.

9 Japo niliwatawanya kati ya mataifa,hata hivyo, watanikumbuka wakiwa humo.Nao pamoja na watoto wao wataishina kurudi majumbani mwao.

10 Nitawarudisha kutoka nchini Misri,nitawakusanya kutoka Ashuru;nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni,nao watajaa kila mahali nchini.

11 Watapitia katika bahari ya mateso,nami nitayapiga mawimbi yake,na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka.Kiburi cha Ashuru kitavunjwana nguvu za Misri zitatoweka.

12 Mimi nitawaimarisha watu wangu,nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14