10 “Pokea zawadi za watu walio uhamishoni zilizoletwa na Heldai, Tobia na Yedaya. Nenda leo hii nyumbani kwa Yosia, mwana wa Sefania ambamo watu hao wamekwenda baada ya kuwasili kutoka Babuloni.
11 Utachukua fedha na dhahabu hiyo, utengeneze taji ambalo utamvika kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki,
12 na kumwambia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Hapa pana mtu aitwaye Tawi. Yeye atastawi hapo alipo na kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.
13 Yeye ndiye atakayelijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu Atapewa heshima ya kifalme na kuketi kwenye kiti chake cha enzi kuwatawala watu wake. Karibu na kiti cha enzi cha mtawala huyo, atakaa kuhani mkuu, nao wawili watafanya kazi pamoja kwa amani.
14 Taji hilo itahifadhiwa katika hekalu langu kwa heshima ya Heldai, Tobia, Yedaya na Yosia mwana wa Sefania.’
15 “Watu wanaokaa nchi za mbali watakuja kusaidia kulijenga hekalu langu mimi Mwenyezi-Mungu.” Nanyi mtajua kwamba Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ndiye aliyenituma kwenu. Haya yote yatatukia kama mkiitii sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.