1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi?
3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema,Dhabihu na toleo hukutaka,Lakini mwili uliniwekea tayari;