4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
5 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,Ndiwe mwanangu,Mimi leo nimekuzaa.
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani mileleKwa mfano wa Melkizedeki.
7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;
9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.