24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.
25 Maana Daudi ataja habari zake,Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote,Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.
26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa,ulimi wangu ukafurahi;Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.
27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.
28 Umenijuvisha njia za uzima;Utanijaza furaha kwa uso wako.
29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.
30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;