31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.
33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.
34 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema,Bwana alimwambia Bwana wangu,Keti upande wa mkono wangu wa kuume.
35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.
36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?