1 Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.
2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.
3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?
4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.
5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.