44 Lakini Pilato akastaajabu, kwamba amekwisha kufa. Akamwita yule akida, akamwuliza kwamba amekufa kitambo.
45 Hata alipokwisha kupata hakika kwa yule akida, alimpa Yusufu yule maiti.
46 Naye akanunua sanda ya kitani, akamtelemsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.
47 Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekw