9 Na watu waliokula wapata elfu nne. Akawaaga.
10 Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda pande za Dalmanutha.
11 Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.
12 Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.
13 Akawaacha, akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.
14 Wakasahau kuchukua mikate, wala chomboni hawana ila mkate mmoja tu.
15 Akawaagiza, akasema, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.