22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,
23 Tazama, bikira atachukua mimba,Naye atazaa mwana;Nao watamwita jina lake Imanueli;Yaani, Mungu pamoja nasi.
24 Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe;
25 asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.