Mt.
Sura 11:9-15
Swahili Union Version
9Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii.
10Huyo ndiye aliyeandikiwa haya,Tazama, mimi namtuma mjumbe wanguMbele ya uso wako,Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye.
12Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
13Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana.
14Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja.
15Mwenye masikio, na asikie.