Mt.
Sura 13:3-9
Swahili Union Version
3Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.
4Hata alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
5nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara zikaota, kwa udongo kukosa kina;
6na jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.
9Mwenye masikio na asikie.