4 Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
5 Nao wanafunzi wakaenda hata ng’ambo, wakasahau kuchukua mikate.
6 Yesu akawaambia, Angalieni, jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.
7 Wakabishana wao kwa wao, wakisema, Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.
8 Naye Yesu akafahamu, akawaambia, Mbona mnabishana ninyi kwa ninyi, enyi wa imani chache, kwa sababu hamna mikate?
9 Hamjafahamu bado, wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa wale elfu tano, na vikapu vingapi mlivyoviokota?
10 Wala ile mikate saba kwa watu elfu nne, na makanda mangapi mliyoyaokota?