42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.
43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,
44 Bwana alimwambia Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,Hata niwawekapo adui zakoKuwa chini ya miguu yako?
45 Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?
46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.