Mt.
Sura 25:11-17
Swahili Union Version
11Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
12Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
13Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.
14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
16Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
17Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.