Mt.
Sura 27:41-47
Swahili Union Version
41Kadhalika na wale wakuu wa makuhani wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe.
42Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
43Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.
44Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.
45Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hata saa tisa.
46Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
47Na baadhi yao waliohudhuria, waliposikia, walisema, Huyu anamwita Eliya.