3 Heri walio maskini wa roho;Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 Heri wenye huzuni;Maana hao watafarijika.
5 Heri wenye upole;Maana hao watairithi nchi.
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki;Maana hao watashibishwa.
7 Heri wenye rehema;Maana hao watapata rehema.
8 Heri wenye moyo safi;Maana hao watamwona Mungu.
9 Heri wapatanishi;Maana hao wataitwa wana wa Mungu.