1 Alipokwisha kusema hayo, Yesu alitoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng’ambo ya kijito Kedroni, palipokuwapo bustani; akaingia yeye na wanafunzi wake.
2 Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
3 Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta?