27 BWANA naye akamwamuru malaika; naye akaurudisha upanga wake alani mwake tena.
28 Wakati huo, Daudi alipoona ya kwamba BWANA amemwitikia katika kiwanja cha Arauna, Myebusi, ndipo hutoa dhabihu huko.
29 Kwa maana ile maskani ya BWANA, aliyoifanya Musa jangwani, na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, vilikuwapo wakati huo mahali pa juu pa Gibeoni.
30 Wala Daudi hakuweza kwenda mbele yake ili kumwuliza Mungu; kwa sababu aliona hofu kwa ajili ya upanga wa yule malaika wa BWANA.