1 Ndipo Daudi akasema, Hii ndiyo nyumba ya BWANA Mungu, na hii ndiyo madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa Israeli.
2 Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu.
3 Daudi akaweka akiba tele ya chuma kwa misumari ya tarabe za malango, na kwa mafungo; na ya shaba akiba tele isiyo na uzani;
4 na mierezi isiyo na idadi; kwa kuwa Wasidoni na watu wa Tiro wakamletea Daudi mierezi tele.