1 Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.
2 Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.
3 Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.
4 Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;
5 na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.