12 Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.
13 Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
14 Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.
15 Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.
16 Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.
17 Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18 Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.