18 Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.
19 Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
20 Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21 Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.
22 Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23 Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.
24 Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.