29 Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza;
30 na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.
31 Na hawa ndio watu aliowaweka Daudi juu ya kazi ya kuimba katika nyumba ya BWANA, sanduku lile lilipokwisha pata mahali pa kustarehe.
32 Nao wakafanya kazi yao ya kuimba mbele ya maskani ya hema ya kukutania, hata Sulemani alipokuwa amejenga ile nyumba ya BWANA huko Yerusalemu; pia wakaisimamia huduma yao sawasawa na zamu zao.
33 Na hawa ndio waliofanya huduma pamoja na wana wao. Katika wana wa Wakohathi; Hemani mwimbaji, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli;
34 mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu;
35 mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai;