21 Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana.
22 Daudi akajibu, akasema, Litazame fumo hili, Ee mfalme! Kijana mmoja na avukie huku, alitwae.
23 Naye BWANA atamlipa kila mtu haki yake, na uaminifu wake; maana BWANA amekutia mikononi mwangu leo, nami nalikataa kuunyosha mkono wangu juu ya masihi wa BWANA.
24 Tena, angalia, kama vile maisha yako yalivyokuwa na thamani machoni pangu, kadhalika na maisha yangu na yawe na thamani machoni pa BWANA, akaniokoe katika shida zote.
25 Ndipo Sauli akamwambia Daudi, Ubarikiwe, Daudi, mwanangu; utatenda mambo makuu, tena hakika yako utashinda. Basi, Daudi akaenda zake; Sauli naye akarudi kwao.