11 Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA.
12 Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.
13 Tazameni, nitawalemea ninyi,Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.
14 Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio;Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake;Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;
15 Wala apindaye upinde hatasimama;Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka;Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;
16 Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaaAtakimbia uchi siku ile, asema BWANA.