16 Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.
17 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
18 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo,
19 ndipo itakapokuwa ya kwamba hapo mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsongezea BWANA sadaka ya kuinuliwa.
20 Katika unga wenu wa kwanza wa chenga-chenga mtasongeza mkate uwe sadaka ya kuinuliwa; vile vile kama mfanyavyo sadaka ya kuinuliwa ya sakafu ya kupuria nafaka, ndivyo mtakavyoiinua.
21 Malimbuko ya unga wenu mtampa BWANA sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.
22 Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote BWANA aliyomwambia Musa,