31 Kwa sababu amelidharau neno la BWANA, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.
32 Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato.
33 Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote.
34 Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.
35 BWANA akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya marago.
36 Basi mkutano wote wakampeleka nje ya marago, nao wakampiga kwa mawe, akafa; kama BWANA alivyomwagiza Musa.
37 Kisha BWANA akasema na Musa, na kumwambia,