20 Kisha akamwangalia Amaleki, akatunga mithali yake, akasema,Amaleki alikuwa ni wa kwanza wa mataifa;Lakini mwisho wake atafikilia uharibifu.
21 Kisha akamwangalia Mkeni, akatunga mithali yake, akasema,Makao yako yana nguvu,Na kitundu chako kimewekwa katika jabali.
22 Pamoja na haya Wakeni wataangamizwa,Hata Ashuru atakapokuchukua mateka.
23 Akatunga mithali yake akasema,Ole wao! Ni nani atakayepona, Mungu atakapofanya haya?
24 Lakini merikebu zitakuja kutoka pwani kwa Kitimu,Nazo zitamtaabisha Ashuru, na Eberi zitamtaabisha,Yeye naye atafikilia uharibifu.
25 Basi Balaamu akainuka, akaondoka na kurudi mahali pake; Balaki naye akaenda zake.