15 Musa akawauliza, Je! Mmewaponya wanawake wote hai?
16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie BWANA dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa BWANA.
17 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye.
18 Lakini hao watoto wote wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye, mtawaweka hai kwa ajili yenu.
19 Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya marago muda wa siku saba; mtu awaye yote aliyemwua mtu, na awaye yote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.
20 Na katika habari ya kila nguo, na kila kitu kilichofanywa cha ngozi, na kazi yote ya singa za mbuzi, na vyombo vyote vilivyofanywa vya mti, mtajitakasa wenyewe;
21 Kisha Eleazari kuhani akawaambia waume wa vita wote waliokwenda vitani, Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyomwagiza Musa;