39 Na punda walikuwa thelathini elfuna mia tano, katika hao kodi ya BWANA ilikuwa punda sitini na mmoja.
40 Na wanadamu walikuwa watu kumi na sita elfu; katika hao sehemu ya BWANA ilikuwa ni watu thelathini na wawili.
41 Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
42 Tena katika hiyo nusu iliyokuwa ya wana wa Israeli, ambayo Musa aliitenga na watu waliokwenda vitani,
43 (basi hiyo nusu ya mkutano ilikuwa ni kondoo mia tatu na thelathini na saba elfu na mia tano,
44 na ng’ombe thelathini na sita elfu,
45 na punda thelathini elfu, na mia tano,