28 Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana.
29 Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;
30 au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za BWANA, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote.
31 Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.