20 naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kitu hicho ni kitakatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa, na paja la kuinuliwa; kisha baadaye Mnadhiri ana ruhusa kunywa divai.
21 Sheria ya Mnadhiri awekaye nadhiri ni hiyo, tena ni sheria ya sadaka yake atakayomtolea BWANA kwa ajili ya kujitenga kwake, pamoja na vitu vile ambavyo aweza kuvipata zaidi; kama nadhiri yake awekayo ilivyo, ndivyo impasavyo kufanya kwa kuiandama sheria ya kujitenga kwake.
22 Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
23 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Hivi ndivyo mtakavyowabarikia wana wa Israeli; mtawaambia;
24 BWANA akubarikie, na kukulinda;
25 BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;
26 BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.