36 Siku ya tano Shelumieli mwana wa Suri-shadai, mkuu wa wana Simeoni;
37 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
38 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;
39 na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;
40 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
41 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Shelumieli mwana wa Suri-shadai
42 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, mkuu wa wana wa Gadi