52 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
53 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Elishama mwana wa Amihudi.
54 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, mkuu wa wana wa Manase;
55 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
56 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilichojaa uvumba;
57 na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;
58 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;