81 na ng’ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa;
82 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi;
83 tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng’ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Ahira mwana wa Enani.
84 Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili;
85 kila sahani ya fedha uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na kila bakuli uzani wake ni shekeli sabini; fedha yote ya vile vyombo ilikuwa shekeli elfu mbili na mia nne, kwa shekeli ya mahali patakatifu;
86 na vijiko vya dhahabu vilivyojaa uvumba kumi na viwili, uzani wake kila kijiko shekeli kumi, kwa shekeli ya mahali patakatifu; dhahabu yote ya vile vijiko ilikuwa shekeli mia na ishirini;
87 ng’ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng’ombe waume kumi na wawili, na hao kondoo waume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo waume wa mwaka wa kwanza walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi waume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;