2 BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
3 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;
4 Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaikaAkashinda; alilia, na kumsihi;Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
5 Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;BWANA ndilo kumbukumbu lake.
6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
7 Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.
8 Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.