6 Watakwenda na makundi yao ya kondoo na ng’ombe wamtafute BWANA; lakini hawatamwona; amejitenga nao.
7 Wametenda kwa hila juu ya BWANA; maana wamezaa wana wageni; sasa mwezi huu uandamao utawala pamoja na mashamba yao.
8 Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-Aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!
9 Efraimu atakuwa ukiwa siku ya kukemewa; katika kabila za Israeli nimetangaza habari itakayotokea halafu bila shaka.
10 Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.
11 Efraimu ameonewa, amesetwa katika hukumu, kwa sababu alikuwa radhi kufuata ubatili.
12 Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda.