2 BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;Naye amekuwa wokovu wangu.Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
3 BWANA ni mtu wa vita,BWANA ndilo jina lake.
4 Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini,Maakida yake wateule wamezama katika bahari ya Shamu.
5 Vilindi vimewafunikiza,Walizama vilindini kama jiwe.
6 BWANA, mkono wako wa kuume umepata fahari ya uwezo,BWANA, mkono wako wa kuume wawaseta-seta adui.
7 Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea,Wapeleka hasira yako, nayo huwateketeza kama mabua makavu.
8 Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa,Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa chungu,Vilindi vikagandamana ndani ya moyo wa bahari.