18 Usimwache mwanamke mchawi kuishi.
19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.
20 Mtu atakayemchinjia sadaka mungu ye yote, isipokuwa ni yeye BWANA peke yake, na angamizwe kabisa.
21 Usimwonee mgeni, wala kumtendea jeuri; kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
22 Usimtese mjane ye yote aliyefiwa na mumewe, wala mtoto yatima.
23 Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
24 na hasira yangu itawaka moto, nami nitawaua ninyi kwa upanga; na wake wenu watakuwa wajane, na watoto wenu mayatima.