28 na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri.
29 Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa BWANA kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo BWANA aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa.
30 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, BWANA amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina;
32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,
33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.
34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.