24 Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.
25 Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.
26 Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.
27 Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa.
28 Akalitia pazia la mlango wa maskani.
29 Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
30 Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.