1 Ndipo BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao, umwambie, BWANA, Mungu wa Waebrania, yuasema, Wape ruhusa watu wangu ili waende wanitumikie.
2 Kwani ukikataa kuwapa ruhusa waende, na kuzidi kuwazuia,
3 tazama, mkono wa BWANA u juu ya wanyama wako wa mifugo walioko kondeni, juu ya farasi, na juu ya punda, na juu ya ngamia, na juu ya ng’ombe, na juu ya kondoo; kutakuwa na tauni nzito sana.
4 Kisha BWANA atawatenga wanyama wa Israeli na wanyama wa Misri; wala hakitakufa kitu cho chote cha wana wa Israeli.
5 Naye BWANA akaweka muda, akasema, Kesho BWANA atalifanya jambo hili katika nchi.