9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10 Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi?Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.
11 Hekima ni njema, mfano wa urithi;Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.
12 Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
13 Tafakari vema kazi yake Mungu; kwa sababu ni nani awezaye kukinyosha kitu kile alichokipotosha yeye?
14 Siku ya kufanikiwa ufurahi,Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake.
15 Mambo hayo yote nimeyaona mimi katika siku za ubatili wangu, yuko mwenye haki apoteaye katika haki yake, yuko na mtu mwovu azidishaye maisha yake katika udhalimu wake.