2 Mimi nasema hivi, Uishike amri ya mfalme; na hiyo kwa sababu umeapa kwa Mungu.
3 Usifanye haraka kutoka mbele ya uso wake; usiendelee kufanya lililo baya; maana yeye hufanya lo lote limpendezalo.
4 Kwa kuwa neno la mfalme lina nguvu; naye ni nani awezaye kumwambia huyo, Wafanya nini?
5 Aishikaye amri hatajua neno baya;Na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu.
6 Kwa maana kwa kila shauri kuna wakati na hukumu; kwa sababu mashaka ya mwanadamu yaliyo juu yake ni makubwa;
7 kwa kuwa hajui yatakayokuwako; kwa maana ni nani awezaye kumweleza jinsi yatakavyokuwa?
8 Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho;Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa;Wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile;Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.