16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng’ombe, na punda waume, na watumwa, na wajakazi, na punda wake, na ngamia.
17 Lakini BWANA akampiga Farao na nyumba yake mapigo makuu, kwa ajili ya Sarai, mkewe Abramu.
18 Ndipo Farao akamwita Abramu, akasema, N’nini hili ulilonitendea? Mbona hukuniambia ya kuwa huyo ni mkeo?
19 Mbona ulisema, Huyo ni umbu langu, hata nikamtwaa kuwa mke wangu? Basi sasa, huyo mke wako umchukue, uende zako.
20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.