1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.